Thursday 6 March 2014

Diva na Gk kulikoni tena??

Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa matukio ya mastaa mbalimbali Bongo, basi utakuwa sio mgeni kabisa na story hii... mwanzoni kabisa mwa mwezi February kuna uvumi ulizuka kuwa Diva Loveness Love mtangazaji wa Clouds FM kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na aliyewahi kuwa mkali wa bongo fleva kwenye miaka ya 2000's, King Crazy GK rais wa East Coast Team, kundi lililokuwa linaundwa na AY, Mwana FA, Snare, Pauline Zongo na GK.

Baada ya story hizo kuenea sana ikabidi mzee wa fununu kutoka lile gazeti la mokorokocho "Soud Brown" akaamua kumvutia waya mtu mzima GK na kuweza kumuuliza kuhusu story hizo kama zinaukweli wowote, ila GK alikataa na kusema hawana mahusiano yoyote zaidi ya kuwa washkaji tu.

Ila hii ya leo kidogo inautata baada ya Diva kupost picha wakiwa na GK somewhere, na zaidi ni status iliyoisupport hiyo post ndio kidogo imeleta maswali juu ya story za awali zinazowahusu wawili hao. "Selfie #US ... Me and My King.... My GK .. My baby.. wit this weather.. cuddling is a must .. We need a baby au?! hahaa Basi. We love you guys. love East Coast Team".

No comments: