Saturday 28 December 2013

Takwimu mbalimbali (2013) kuhusu mastaa wa bongo

Msanii wa kiume mwenye mkwanja mrefu

 
Kwa mujibu wa Takwimu zilizopigwa na team_Kibongobongo, inasemekana kuwa msanii Diamond Platnumz ndiye anayeshikilia nafasi ya kuwa msanii wa kwanza kuingiza kipato kikubwa kwa kupitia sanaa yake ya muziki. Diamond amekuwa akiongoza kwa kupiga show nyingi kwa mwaka 2013, pia amekuwa akiongoza kama msanii anayedaka mkwanja mrefu kwa kupitia show hizo ambazo amekuwa akipiga ndani na nje ya nchi mbalimbali zikiwemo, UK,US,CONGO,CHINA,INDIA na sehemu kibao. Hata hivo Diamond ameweza kuingiza mkwanja kwa kupitia caller-tune za kwenye mitandao ya simu kwa kulipwa mkwanja mnene na baadhi ya makampuni yanayojihusisha na dili za kuuza miito ya simu (caller-tune). Pia kwa kupitia dili kibao za kusign mikataba na baadhi ya makampuni kama Coca Cola kuwa balozi wa Coca Cola, Vodacom na nyingine mkali huyo ameweza kuwa kinara kwa mwaka 2013.

Msanii wa kike mwenye mkwanja mrefu

Vile vile kwa mujibu wa takwimu zetu tumegundua kuwa mwanadada Lady Jay Dee ndiye msanii pekee wa kike anayemake mkwanja mrefu kwa mwaka 2013. Takwimu hizi zimebaini ilo baada ya kuangalia show anazopiga mwanadadashost JIDE kwa wiki na kuweza kuingiza kisu kirefu...pia kulingana na takwimu zilizowahi kufanywa na baadhi ya vyombo vya habari miaka kadhaa ya nyima na kuweza kugundua kuwa JIDE anashikilia namba hiyo kwa kuweza kumiliki baadhi ya invetments kama kampuni ya maji japo kuwa haikuweza kusimama kwa kiasi kikubwa, pia anamiliki Nyumba Lounge ambayo inamuingizia Salary ya kutosha na kuweza kuzichanga vya kutosha na kunenepesha Account yake.

Staa anayeandikwa sana magazetini

Nafasi hii imeshikiliwa na super beautiful Lady a.k.a Beautiful Onyinye au The BossLady Wema Isack Sepetu. Wema ameweza kushika nafasi hiyo kwa kuwa ameongoza kuandikwa kwenye magazeti kwa mwaka 2013 haijalishi ni habari nzuri au mbaya isipokuwa yamuhusu yeye. Pia nafasi hiyo imefuatiwa na msanii Diamond ambapo nayeye ameweza kuandikwa sana kwenye magazeti kufuatia kasumba lake na Wema na Penny lililosumbua vichwa vya wapenzi na wadau wengi wa mastaa hao.

Staa mdogo aliyechipukia

Napozungumzia staa aliyechipukia namaanisha aliyeweza kuingia kwenye sanaa yeyote ile na kuweza kuteka soko kwa kupendwa na jamii na kuzidi kufanya vizuri....hivyo basi kwa mwaka 2013 nafasi ya staa mdogo aliyeweza kufanya vizuri team_Kibongobongo tumemdondoshea kijana Young Killa Msodoki. Young Killa ni staa mdogo aliyeweza kuingia kwenye game ya muziki hususani wa Hip Hop kufuatia shindano la super nyota lililoandaliwa na Clouds FM na kuweza fanya vizuri na kuibuka kinara wa shindano hilo. Young Kila aliingia kwenye game na kufanya vizuri mwanzoni mwa mwaka 2013 kwa kuachia kibao cha Dear Gambe alichoshirikiana na mkali Belle 9. Kibao hicho kimeweza pendwa na wadau wengi wa muziki huo na kumfanya kijana awezeku'shine kwenye show mbalimbali zikiwemo Fiesta na nyingine kibao.

mcheza filamu bora za kibongo

Nafasi hii imekamatwa na Jacob Steven a.k.a BONGE LA BWANA...Jamaa amekuwa akichaguliwa mara kwa mara kupitia media mbalimbali kuwa ndiye mcheza filamu mzuri wa BONGO MOVIE kwa kuwa na kipaji cha pekee kwenye kuziteka hisia za wadau na wapenzi wa filamu hizo. Pia nafisi hii imefuatiwa na mwanadada Wema Sepetu kuwa staa mzuri wa kucheza filamu za kibongo.

Mtangazaji nayesikilizwa na wengi

Kwa kuangalia vigezo mbalimbali kama kuangali ukurasa na account za baadhi ya watangazaji kwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Instagram...takwimu zilizopo ni kwamba nafasi hii imenyakuliwa na Millard Ayo mtangazaji wa Clouds FM pia anamiliki website yake (Millard Ayo.com). Mirald amekuwa akifuatiliwa kwa maana ya kusikilizwa na kusomwa sana habari zake na jamii kubwa wakiwemo wazee na vijana. Millard ameweza kushika nafasi hiyo kutokana na umahiri wa utangazaji wake na kujituma katika kutafuta habari. Kama umekuwa ukimfuatilia, Millard ameshasafiri sehemu mbalimbali za nje na ndani ya Tanzania kwa ajili ya kukusanya habari, mfano habari kuhusu kifo cha Abert Mangwea na kulazwa kwa M 2 za P, habari kuhusu babu wa Loliondo na habari nyingi zinazohusu jamii inayotuzunguka. Kwa tetesi zilizopo ni kuwa jamaa alishatamaniwa na BBC Swahili inayofanya matangazo yake nchini ujerumani akafanyekazi isipokuwa uongozi wa Clouds FM ukamtangazia dau nene na kuweza kumbakisha mkali huyo.


ITAENDELEA...

1 comment:

Anonymous said...

Mshamba diamond!!!!!!!.