Tuesday 24 September 2013

Watu wawili wakamatwa na maiti ikiwa na dawa za kulevya

Watu wawili wakamatwa wakiwa na maiti iliyokutwa na dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleimani Kova amesema ugunduzi huo ulibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari wa hospitali ya taifa Muhimbili wakishuhudiwa na polisi pamoja na baadhi na ndugu wa marehemu ambapo ameelezea marehemu alikutwa na hati za dharura za kusafiria nchi za nje na kuwa uchunguzi zaidi unafanyika kubaini mtandao mzima wa usafirishaji wa dawa hizo uliomuhusisha marehemu.
Katika tukio lingine kamanda Kova amesema jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kuwa mtumishi wa wizara ya afya na ustawi wa jamii aliyekamatwa katika hospitali ya taifa Muhimbili akiwa amevalia mavazi ya kidaktari pamoja na nyara mbalimbali zenye nembo ya hospitali hiyo kwa lengo la kuwaibia watu.
Kutokana na tukio la ugaidi nchini Kenya kamanda Kova amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulizi maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu wengi na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi watakapo baini mtu au kikundi cha watu wanaowatilia shaka.

No comments: