Tuesday 3 September 2013

Alichosema Shedy Clever kuhusu Dayna kulalamika kuibiwa wimbo na Diamond

Ni baada ya sakata la kuibiana nyimbo lililochokua takribani siku kadhaa sasa kwa  msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange.
Baada ya Dayna kufunguka yake kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo instagram kwa madai ya yeye kuibiwa wimbo wa Number One na msanii Diamond, ambapo sakata hilo lilimuhusisha na produza aliyesuka beat ya wimbo huo, Shedy Clever kutoka Burn recods. Hivyobasi Chanzo chetu kikamtafuta Producer huyo ili kujua ukweli juu ya kitu hiki.
Shedy alisema “Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe, alivyokuja Dayna akaupenda ule mdundo, na mimi sikumnyima akafanya demo lakini hakulipia kabisa. Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya. Kuna siku Diamond akaja studio pale, akataka kusikia midumdo nikacheza midundo mbalimbali ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna alifanya demo. Mimi nikampigia Dayna na kumuelezea kwamba diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat, Dayna akakubali kabisa, sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali kabisa. Mimi sina cha kusema zaidi ila ukweli upo hivyo..." alifunguka hayo producer huyo.
CHANZO: TIZNIZ.COM

No comments: