Saturday 3 August 2013

Wema ajaza watu mahakamani

Msanii wa Bongo Movie ambaye kwasasa alifunguka kuwa anataka ajaribu kuingia kwenye game ya muziki, Wema Abraham Sepetu, Jana amekuwa kivutio cha watu katika mahakama ya Kawe Jijini DSM baada ya kuja na kundi la wapambe wake wakiwa na gari tofauti.

Bibie huyo anayekabiliwa na kesi ya kumtukana na kutaka kumpiga makofi meneja wa Hotel moja ya jijini DSM, Bw. Goodlucky Kuyumbu kwa mujibu wa Global Publisher. Alikuja na gari yake ya kifahari aina ya Q-7 AUDI huku wapambe wakiwa kwenye gari mbili tofauti ambazo ni Toyota Opa na Toyota Haice...Tukio hilo lilionekana kuwa ni la kustaajabisha kwani walimbwende hao walikuja kwa mbwembwe na huku wakiwa hawana sura za kuwa na wasiwasi juu ya kesi hiyo.

Hata hivyo kesi hiyo ilihailishwa hadi August, 20 mwaka huu baada ya upande wa mtoa mashtaka kutakiwa kuleta ushahidi wa kutosha.
Wema akiwasili
 Kajala naye alikuwepo kumpa support Wema
 Hii ndio ndinga ya mwanadada huyo

No comments: