Saturday 20 July 2013

Picha za utengenezaji wa Video ya "Uzuri wako" ya Jux

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, Jux ambaye yupo nchini China kimasomo japo haikuweza kufahamika ni chuo gani anachosoma mkali huyo wa RnB na anasomea nini. Mwanzoni mwa mwezi huu ametuma baadhi ya picha za utengenezaji wa video ya wimbo wake wa "Uzuri wako". Wimbo huo ambao kwa sasa umekuwa ukibamba kwa kuwa na ujumbe mzuri na vionjo vilivyotumika katika kutengeneza wimbo huo kuwa vya kipekee kabisa.

Hata hivyo haikuweza kufahamika ni lini video hiyo itakuwa tayari na imetengenezwa na kampuni gani japo kwa muonekano wa picha hizi zinaonesha video hiyo imeshootiwa nchini China na msichana aliyecheza humo pia ni wakizungu.

No comments: