Saturday 20 July 2013

Askari wa Tanzania aliyekamatwa huko DRC

HABARI TULIZOZIPATA KUPITIA MTANDAO WA WAASI WA M23 WANADAI WAMEMKAMATA ASKARI WA KITANZANIA HUKO MASHARIKI MWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO. Hiyo hapo pichani ni passport ya askari huyo, ajulikanae kwa jina la CHRISTOPHER GEORGE YOHANA... Soma zaidi walichoandika, hao waasi wa M23, soma taratibu maana Kiswahili walichotumia ni kigumu kidogo kuelewa...

''leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania
ambaye tulikamata''

No comments: