Sunday 9 June 2013

R.I.P My Brother Frank

Frank na pikipiki yake enzi za uhai wake
Leo majira ya saa mbili asubuhi teamKibongobongo tumepokea taarifa za kusikitisha kutoka kwa jamaa yetu wa karibu kuwa mmoja wa jamaa yetu pia ni mdau mkubwa wa Blog hii, Frank Ndakidemi aliyekuwa akisoma chuo cha CBE - Dodoma amefariki jana kwa ajali ya pikipiki.

Chanzo kimesema kuwa Frank aliivamia daladala yenye kufanya safari zake Nkhungu - Nanenane, mkoani Dodoma akiwa kwenye pikipiki yake na kuumia vibaya kiasi cha kumfanya apoteze maisha.

TeamKibongobongo tumesikitishwa sana na msiba huu, kwani hata wiki bado haijakatika tangu tumpoteze mdau wetu mwingine, Steven Mhina aliyefariki June 2 kwa ajali ya pikipiki pia.

Tunatanguliza salamu zetu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wote wa karibu na marehemu pia pole sana wanafunzi wa Ruaha waliosoma na marehemu na wanachuo wa CBE-DODOMA. 
Pikipiki yake na gari alilogongananalo

No comments: