Wednesday 8 May 2013

Muonekano mpya wa studio ya Bongo Record

Hii ni baada ya marekebisho yaliyofanywa kwenye studio ya Bongo Record iliyochini ya producer P-Funk Majani. P Funk amewahakikishia mashabiki wake kuwa kwa sasa anakuja upya kabisa hivyo wawe tayari kupokea ngoma zitakazopikwa kutoka kwenye studio hiyo.
P-Funk ni producer aliyewika sana miaka ya nyuma kwa kupika ngoma Kali zilizotamba miaka hiyo kama ZEZE ya TID, CHEZA KWA STEP ya Ngwair, GETHO LANGU ya Ngwair, pia amepika Album kibao zilizofanya vizuri sokoni ikiwemo album ya A.K.A MIMI ya Ngwair, NINI CHANZO,UGALI zote za Juma Nature, album ya ULIMWENGU NDIO MAMA ya Jmoe, album ya Soggy na nyingine nyingi.
Pia P-Funk Majani ameshanyakuwa tuzo za kuwa mpishi bora wa nyimbo kwa yakribani mara tatu kupitia tuzo zitolewazo na Kilimanjaro Premium Lager zijulikanazo kama TANZANIA KILL MUSIC AWARDS.

No comments: