Wednesday 17 April 2013

R.I.P legendary Bi Kidude

Mwanamuziki maarufu na mwenye umri mkubwa kuliko nchini Tanzania, Bi Kidude, amefariki dunia leo hii akiwa Zanzibar, alikuwa anaumwa na alipowahishwa hospitali haikuwa bahati.
Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mpwa wake Baraka Abdulrahman Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini kutokana na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.
Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.
Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa ikizorota kiasi cha serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani kuburudisha japokuwa alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi Februari mwaka huu. Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake Zanzibar.

No comments: