Tuesday 16 April 2013

mlipuko uliotokea jijini boston

Jana kumetokea mlipuko kwenye mashindano ya riadha jijini Boston - Marekani nakuua watu kadhaa na kujeruhi wengine.

Kupitia baadhi ya vyombo vya habari nchi humo vimeripoti kuwa milipuko imetokea sehemu tofauti kwenye eneo ambako kulikuwa na mashindano hayo. Milipuko miwili imetokea jirani kabisa na mstari wa kumalizia mashindano hayo yaliokuwa yakiendelea ya riadha, na pia mlipuko mwingine watatu umetokea nje ya library ya JFK na kurepotiwa kuwa hadi sasa yadaiwa watu waliopoteza maisha ni wawili na majerui ni 23 kwenye milipuko hiyo miwili.

Rais Obama amesema machache kuhusu tukio hilo jana kupitia vyombo vya habari Ikulu, amesema jeshi la polisi limeongeza jitihada zaidi hususani kwenye masuala ya usalama na pia kwenye suala la uokoaji wanajitahidi kwa kila hali.
Amewaomba wananchi wawe na utulivu wakati jeshi na wanausalama wanafanya kazi zao za kiusalama kuhusiana na tukio hilo la kusikitisha.

Obama akizungumzia mlipuko huo

baadhi ya picha za tukio hilo

No comments: