Friday 19 April 2013

beckham awa balozi wa SKY TV


Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham ambaye kwa sasa anakipiga huko Ufaransa kwenye klabu ya Paris St Germain amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuwa balozi wa kituo cha televisheni cha Sky .
Katika mkataba huo Becks atakuwa akilipwa paundi milioni 20 ambapo kazi yake kubwa itakuwa kuotagaza televisheni hiyo na kuipa taswira ya kimataifa .
Mkataba huu kati ya Becks na Sky Tv inayomilikiwa na bilionea wa zamani ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wanahisa wa Manchester United kwenye miaka ya 90 Rupert Murdoch ni jibu kwa mahasimu wa Sky Tv Televisheni ya BT Sports ambao walimsainisha nyota wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale kama balozi wake kabla ya kuzinduliwa kwake rasmi baadaye mwaka huu.
Katika mikataba hiyo nyota hao wawili watafanya kazi za kutangaza huduma za televisheni hizo zinazohusiana zaidi na matangazo ya michezo ya ligi kuu ya England huku wakifanya kazi kama wachambuzi maalum wa baadhi ya mechi.
Pamoja na matangazo na uchambuzi Beckham atakuwa na jukumu la kuwa mwalimu wa masuala ya kimaisha kwa wanamichezo chipukizi watakaokuwa wanalelewa kwenye kituo kinachofadhiliwa na Sky TV...

No comments: