Monday 31 December 2012

hii ndio haice iliyowaka moto mkoani iringa

Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayosafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu ya injini.
Ilitokea saa saba mchana december 30 katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo Iringa ambapo shuhuda wa ajali amesema hii daladala ilikua inatokea Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa. 
Mmiliki wa dala dala Ayubu Kabigi amesema amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo lakini amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari lake.

No comments: