Monday 9 July 2012

HABARI KUHUSU SINGLE BOY YA ALLY KIBA

Ni miongoni mwa vipande vya video ya single boy
Ally Kiba                   Diamond
Mwanzoni mwa mwezi march au mwishoni mwa mwezi 
February kama sijakosea, msanii wa bongo fleva 
aliyetamba na nyimbo ya Nakshi nakshi, Sindelela, 
Njiwa na nyingine nyingi Mwanzoni mwa mwa 2007 
na kwa sasa anasumbua na Single boy aliyomshirikisha
 mwanadadashost Lady Jay Dee.
Swali "JE, UNAJUA KWANINI HII NYIMBO 
IKAITWA SINGLE BOY KANA KWAMBA 
INAMUHUSU NA SINGLE GIRL AU IMEIMBWA
 NA JIDEE KUHUSU SINGLE GIRL??
Jibu " ya kwamba....kuna story zinazoeleza kuwa hii
 ngoma ilitakiwa afanye na Diamond na kuhusu only
 single boy, so kwa zile sababu zilizo nyuma ya pazia
 jamaa akachomoa ndipo mtu mzima akuamua 
kumtupia mwanadadashost Jay D"
Kufuatia chanzo cha habari "Bongo 5"
kililiport "Inasemekana kwamba kuna beef kati 
ya masuperstars wa muziki wa kizazi kipya nchini
 Ali Kiba na Nassib Abdul aka Diamond,
 chanzo cha beef ni kushutumana kufutiana
 vocals katika nyimbo zao.
Habari zinasema kwamba Ali Kiba anadai 
Diamond ndiye aliyeanza utata baada ya kufuta
 sauti yake kwenye rekodi ya Lala Salama 
ambayo alishiriki awali, ila baada ya hiyo 
ngoma kwenda redioni hakuskia sauti yake!

Kwa upande wa Diamond yeye anadai kuwa
 ngoma ya Kiba inayofanya vizuri hivi sasa
 Single Boy walifanya wote ila mwishowe 
akuskia sauti yake na badala yake 
akaskia sauti ya Lady Jay Dee!!

No comments: