Tuesday, 22 May 2012

KUMBUKUMBU YA AJALI YA MV BUKOBA

TZ-MODEL FLAVIANA MATATA ATOA MABOYA 500
Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 
kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, 
Elias Makori (kulia) ikiwa ni kumbukumbu ya 
miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba, 
anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara 
wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani 
Mwanza la Marine Service, Kapten Obadia
 Nkongoki Igoma jijini Mwanza.
Flaviana Matata alishindwa kujizuia na kuangua kilio
 wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 
ya ajali ya meli ya MV Bukoba alipotembelea 
baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha
 katika ajali hiyo yaliyopo Igoma jijini Mwanza 
katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza mama yake mzazi. 
Flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye 
makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza.
Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao 
wakiombea marehemu wa ajali hiyo.

Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ilikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.

Afrika ya kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)

Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)

Vifaa vya uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama walivyozoea kusema)

No comments: