Monday 9 January 2012

WANAFUNZI WA CHUO CHA MIPANGO WATEKETEZA KIBANDA CHA MFANYABIASHARA

Wanafunzi wa chuo cha Mipango (IRDP) - Dodoma course ya "Finance and Investment" mwaka wa tatu, leo majira ya saa saba mchana wamevamia kibanda cha mfanyabiashara jirani na chuo hicho, kwa mujibu wa habari nilizopata ni kwamba wanafunzi hao walichukua jukumu hilo kutokana na kitendo cha kinyama alichofanyiwa mwanafunzi mwenzao kwa kupigwa na kujeruhiwa kwa panga kwenye mdomo na kutolewa jino, kijana huyo ambae ni mfanyabihashara jirani na chuo anaejulikana kwa jina la Daudi, alimjeruhi mwanafunzi huyo kwa tuhuma za kumuhisia kuwa anatembea na mkewe, jambo ambalo sio la kweli kabisa kwa mujibu wa jirani zake wanaojua mpango mzima. Mfanyabihashara huyo alimfananisha kijana huyo kwa kupewa maelekezo yenye kumlenga mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Baraka Kajange.
Wanafunzi hao walichukua jukumu la kukiteketeza kibanda cha mfanyabihashara huyo baada ya kumkosa mtuhumiwa aliyedaiwa kukimbia mahali hapo. Hata hivyo uongozi wa chuo kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mtaa umeridhia kitendo walichokifanya wanafunzi hao kuwa ni mfano kwa watu wenye matendo ya kinyama kama mfanyabihashara huyo.
wanafunzi wakikishughulikia kibanda hicho
maezeka ya kibanda hicho yakiwa yametolewa
kibanda kikiwa kimeshusha chote

 mabati na maezeka yakiteketezwa kwa moto
 
Ujumbe toka kwa wanafunzi hao: "huu ni mwanzo ila ataona mwisho,
na kwa wale wenye roho za kinyama kama bwana Daudi waige waone! 
"CHEZEA MADENT"

1 comment:

lily John said...

lazima ajute manina zake..anacheza na wanafuzi