Sunday, 20 November 2011

KITABU CHA SUGU KIPOTAYARI

Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia chama cha CHADEMA, Joseph Mbilinyi "Sugu" akiwa na kitabu ambacho kinayazungumzia maisha yake (biography) tangu mdogo, harakati zake katika muziki na hatimaye kugombea uwakilishi wa wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hajatamka kitabu kitapatikana madukani lini, kitapatikana katika maduka na wakala gani, wasambazaji ni akina nani, wala mawasiliano ya jinsi ya kukipata.
Nadhani ni hatua mojawapo nzuri na changamoto kwetu Watanzania wote kuwa na tabia ya kupenda kuandika na kujisomea vitabu mbalimbali.
Sina shaka kuwa kitabu kama cha "Sugu" kitakuwa chachu kwa watu wa rika mbalimbali, hasa vijana, ambao wangependa kujifunza mema ya kuigwa katika mapito ya Mheshimiwa Mbilinyi.

Hii ni video inayoonesha na kukielezea kitabu hicho kwa ufasaa

No comments: