Thursday 18 August 2011

BESTA ASANUKA KUHUSU MAISHA YAKE

BESTA
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Besta Prosper Rugeyamu asanuka na kuweka bayana dhidi ya maneno yanayosemwa mtaani na kwenye vyombo vya habari. 
Nanukuu: 
"Fans wangu, nimekuwa nikipata msg nyingi sana mkiniuliza kama nna mtoto au mtoto wangu hajambo. Napenda kuiweka wazi rasmi ili kuondoa UTATA uliopo kama nna mtoto au la. Jibu ni kwamba, sina mtoto bado. Habari zilizowahi kuandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa nilikuwa mjamzito hazikuwa za kweli! Siku ntakayokuwa mjamzito ctaficha, fans wangu mtakuwa number 1 kufahamu. Nawapenda wote, thanx!" ndivyo alivyotupia kwenye wall yake..
Besta ambaye ni mke wa ndoa wa Marlow na wanaishi pamoja.

No comments: