Thursday, 5 December 2013

R.I.P Nelson Mandela "Madiba"

Leo usiku December 05, 2013 imetangazwa rasmi kuwa aliyekuwa rais mpiganaji wa nchi ya Afrika ya Kusini, Nelson Mandela "Madiba" amefariki dunia. Taarifa za kifo cha mpiganaji huyo zimetangazwa na rais wa nchi hiyo Jacob Zuma. Mr Zuma akiongea na South African National TV, amesema "Our Nation has lost its greatest son".

Kundi la watu wameonekana nje ya nyumba ambayo Mandela alipofia huku wengi wakilia, wengine wakiwa wamevaa na kupepea bendera ya chama cha African National Congress. Mandela ameonekana kwenye alaiki ya watu kwa mara ya mwisho 2010 kwenye mashindano ya kuwania kombe la dunia yaliyofanyika nchini humo (Afrika ya kusini).

Mandela amefariki akiwa na umri wa miaka 95, akiwa kama rais wa kwanza wa nchi hiyo na ndiyo mpiganaji aliyeikomboa Afrika ya kusini dhidi ya wakoloni na kupigania vita dhidi ya ubaguzi wa rangi uliyokuwa ukifanya katika nchi hiyo.

Kwamujibu wa taarifa kuhusu mazishi ya Nelson Mandela, yatafanyika siku ya jumaamosi ya wiki ijayo baada ya mwili wake kuletwa Pretoria kwa taratibu za mazishi.

No comments: