Aliyewahikuwa mcheza kikapu maarufu, Dennis Rodman ameongozana na baadhi ya wacheza kikapu wastaafu huko Korea ya Kaskazini jana (January 06).... amesema ameongozana na wacheza kikapu hao huko Korea kwa niaba ya kumuonesha ishara ya upendo Kim Jong-Un kiongozi wa nchi hiyo. Pia amefanya ziara hiyo kwa kuweza kusheherekea sherehe ya kuzaliwa kwa Kim kwa kucheza mechi na timu ya kikapu ya Korea Kaskazini.
Rodman akiwa na Kim Jong-Un
Rodman ameshawishika kufanyahivyo kwa kuwa anamkubali sana Kim na pia anataka kuonesha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili. Rodman amesema haoni tatizo kwa yeye kuongozana na timu hiyo hadi Korea labda tatizo liwepo kwenye masuala ya sheria za taifa hilo.
"Kim was "a nice guy" and that he would not interfere in the North Korea's politics. 'Whatever he [Kim] does political-wise, that's not my job,"... "I just know the fact that, you know, to me he's a nice guy, to
me." alisema Rodman.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema Rodman ameshakwenda huko takribani mara tatu na mara zote amekuwa akifika na kuwa mgeni wa Kim, ameongeza kusema mbali na masuala ya uongozi, Kim ni rafiki yake na wamekuwa wote kwenye masuala ya michezo hususani mpira huo wa kikapu.
Kim Jong-Un ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-iI ambaye kwasasa ni marehemu, amesoma Switzerland na amekuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Chicago Bulls ailiyowahichezea Roman na kuwa mshindi mara tatu wa NBA kwenye miaka ya 1990's.
Kim Jong-Un ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-iI ambaye kwasasa ni marehemu, amesoma Switzerland na amekuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Chicago Bulls ailiyowahichezea Roman na kuwa mshindi mara tatu wa NBA kwenye miaka ya 1990's.
1 comment:
Kim waangalie wamarekani hawana urafiki na mtu inawezekana rodman akawa source wa CIA muda mrefu wamarekani wakamtumia kujuwa mapungufu yako Kwa kutumia interest zako. Take care brother!
Post a Comment