Thursday 19 September 2013

Aki na Pawpaw wamkumbuka baba yao

Sam Loco Efe aliyekuwa mmoja wa waigizaji maarufu nchini Nigeria, leo amekumbukwa na vijana wake AKI na PAWPAW (Chinedu Ikedieze na Osita Ihemewaliowahi kucheza nae baadhi ya filamu akiwa kama baba yao. Vijana hao wamepost ujumbe wa kumkumbuka muigizaji huyo kupitia ukurasa wao wa facebook na kuweka picha iliyokuwa imetumika kwenye moja ya filamu zao walizowahi cheza.

Sam Loco Efe alifariki dunia jumpili ya tarehe 07 august, 2011 kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye blog maarufu inayohusika na soko la filamu nchini Nigeria (NOLLYWOOD BY MINDSPACE) zilireport kuwa Efe alifariki dunia akiwa kwenye process za kucheza filamu iliyopewa jina la Unknown Prophet, mwili wake ulikutwa baada ya mlango wa chumba cha hotel alipokuwa amelala kufunguliwa kwa nguvu. Sam Efe amekufa akiwa na umri wa miaka 66 ni mwenyeji wa Benin, Edo State Nigeria. Mzaliwa wa Enugu, na amekulia Abakaliki...
Sam Loso Efe pia aliweza kuiigiza majukwaani, kwenye vipindi mbalimbali vya luninga na kupitia filamu mbalimbali, na ni mwenyekipaji cha hali ya juu atakumbukwa kwa mengi sana ikiwemo mchango wake wa kurekebisha kiingereza na lugha asilia. Ameshiriki takribani filamu  130 zikiwemo "Heart of stone", "Husband My Foot", "Away Match", "Brain Box" na nyinginezo.

No comments: