Thursday 19 September 2013

Masogange is baaaaaaaack!!

MASOGANGE "aggnesfineassgirl" IS BAAAAACK!!

Kama umechelewa kujua kuhusu ishu ya Masogange....kwa taarifa zilizoenea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ni kuwa mwanadadashosti huyo yuko huru hivi sasa kutoka kwenye ile kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kuhusishwa na ubebaji wa madawa ya kulevya na kuingia nayo nchini Afrika ya kusini.

Agness Gerald maarufu kama Aggy Masogange na mwenzie Melisa Edward walikamatwa Julai 5 mwaka huu nchini humo na kupandishwa kizimbani mnamo August 13 kwa kosa la kukutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.

Kwa mujibu ya taarifa tulizozipata #Team_Kibongobongo ambazo zilitupa matumaini ya kumuona tena Agness akiwa huru ni juu ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu juu ya dawa hizo na kutambua kuwa sio dawa halisi za kulevya isipokuwa ni aina ya madawa ambayo utumiwa kutengenezea madawa ya kulevya...Aina hiyo ya dawa kitaalamu ulinganishwa na mmea unaoitwa "COKE" ambao hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya COCAINE na pia ni mmea unaotumika kutengenezea soda aina ya COCACOLA. Pia utofauti wa dawa izo na dawa halisi za kulevya ni mdogo sana ambao ni kwa element moja.

Hivyo kesi hiyo imekuwa na makali kidogo baada ya taarifa hizo toka kwa wataalamu waliochunguza dawa hizo....kwahiyo kesi kama hiyo yaweza kuwa na dhamana, na ndipo sisi kama #Team_Kibongobongo tulishatarajia kumuona tena Aggy akiwa huru.

#SHIKAMOO_BONGO


Mwanadada Agnes leo hii kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, ameweka picha zake akiwa kwenye mazoezi ya viungo (GYM).

No comments: