
Marehem Chiwoniso
Aliyekuwa mwanamuziki mashuhuri nchini humo ambaye
pia alisifika kwa kucheza ala ya muziki ijulikanayo kama Mbira, ambayo wanaume pekee ndio wanaruhusiwa kuicheza nchini Zimbabwe, Aitwaye Chiwoniso Maraire amefariki dunia. Anasemekana alifariki kutokana na homa ya
mapafu, sasa ni mwaka mmoja tu baada ya aliyekuwa mumewe, Andy Brown, ambaye pia
alisifika kwa muziki wake nchini Zimbabawe kufariki. Walikuwa na watoto
wawili tu.

Chiwoniso na Andy wakiwa na mtoto wao
Chiwoniso amefariki akiwa na umri wa miaka 37 kwa mujibu wa meneja wake....alizaliwa nchini Marekani mwaka 1976, kabla ya kuhamia nchini Zimbabwe akiwa na umri wa miaka saba.
Album yake ya "Ancient Voices" ilimpa sifa tele katika ukumbi wa kimataifa mapema miaka ya 1990 na kuweza kujizolea mamia ya mashabiki nje na ndani ya nchi ya Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment