Thursday 2 May 2013

Wastara akataa kuolewa

Msanii wa filamu nchini, Wastara Juma aliyekuwa mke wa marehemu Sajuki, hivi karibuni amekataa kuolewa baada ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja wa jijini Dar es salaam na kumtaka awe mke wa pili wa kwenye ndoa yake.
Wastara ambaye kwa sasa yupo Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada ya kufiwa na mumewe Sadick Juma Kilowoko "Sajuki" mwezi Januari mwaka huu na amesema hafikirii kabisa suala la kuolewa. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kushauriana na mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia yao. “Mwenyewe alisema alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara kuwa mke mwenzake kwa sababu imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza chanzo hicho. 

Baada ya kuzinyaka habari hizo, kama kawaida yate lilimnyanyulia mkonga mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, akathibitisha kumpigia Wastara. “Lengo langu lilikuwa zuri tu, unajua dini yetu ya Kiislamu inaturuhusu kuolewa wanawake mpaka wanne hivyo niliona ni heri nikae na mwenzangu. “Halikuwa suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na tulishajipanga kwenda kutoa mahari kwao. Nimesikitika sana alivyokataa ila namtakia kila la heri katika maisha yake,” alisema. 

ALICHOJIBU WASTARA 
“Ni kweli nilipigiwa simu na mwanamke wa huko nyumbani (Tanzania), nilimjibu kama ninavyokuambia wewe sasa hivi, kwamba sifikirii kuolewa kwa sasa,” alisema Wastara kwa njia simu alipopigiwa na mwandishi wetu. 

CHANZO; xdeejaz.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment