Thursday 2 May 2013

Kitale awaomba watanzania wampigie kura marehemu Sharo Millionea

Aliyekuwa mtu wa karibu sana na marehemu Sharo Milionea aliyefariki dunia mwezi Septemba mwaka jana, Mussa Kitale alimaarufu kama Kitale Rais wa Mateja leo kupitia mtandao wa kijamii wa facebook amewaomba wale wapenzi na mashabiki wa marehemu Sharo Milionea wampigie kura ili kumuwezesha marehemu Sharo kuchukua tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 zilizopangwa kufanyika mwezi june mwaka huu.
Sharo Milionea amebahatika kuingia katika vipengele viwili kwenye kuwania tuzo hizo, (1) Wimbo bora wa Pop (2) Wimbo bora wa kushirikishwa. Hivyo basi ili kumfanikisha marehemu Sharo kunyakuwa tuzo ya kipengele (1) andika BP3 kisha tuma kwenda 15345, na kumuwezesha kushinda kipengele (2) andika BR1 kisha tuma kwenda 15345.

No comments:

Post a Comment