Thursday 2 May 2013

R.I.P Mac Daddy

Wengi tuliozaliwa miaka ya nyuma kidogo na tulikuwa wafuatiliaji wazuri wa muziki lazima tutakuwa tunakumbuka kundi la Chriss Cross lililosumbua ulimwengu na nyimbo yake ya "Jump" mwaka 1992 likiwa na vijana wawili machachali "Chriss Kelly na Chriss Smith"

Ripoti inasema kwamba Chriss Kelly maarufu kama “Mac Daddy” kutoka kwenye kundi la Kris Kross lililofanya vizuri kwenye miaka ya 90, amefariki dunia May 1 2013 akiwa na umri wa miaka 34 ambapo polisi wamesema alikutwa amefariki na inaonekana ni kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kupitiliza.
Kwa mujibu wa Necole Bitchie, Akini Jeffrey ambae ni producer kutoka kwenye kituo cha 94.5 amesema aliongea na Chris asubuhi ya May 1 kuhusu siku sahihi ya birthday yake baada ya habari kuandikwa kwenye blog kwamba ni May 1 badala ya August 11 ambayo ndio sahihi. Chris alikua mzima na mwenye furaha na aliomba msamaha pia kwa kutotokea kwenye radio interview ya 94.5 february 2013.

kama hukubahatika kuiona moja ya video yao iliyosumbua miaka hiyo, hii hapa pata kuitazama hapa

No comments:

Post a Comment