Friday 3 May 2013

Wanafunzi watano wafa kwa ajali nchini Kenya

Ijumaa ya wiki iliyopita vimetokea vifo vya wanafunzi watano wa shule ya sekondari ya Nambale Boys High school huko Busia, Nairobi nchini Kenya. Wanafunzi hao ambao walikuwa kwenye ziala ya kimasomo ndipo wakapata ajali katikati ya barabara ya Nakuru kwenda Marigat. Ziala hiyo ya kimasomo iliwahusisha wanafunzi wa kidato cha nne peke yake.

Mkuu wa jimbo hilo la Busia Mh. Sospeter Ojaamong na mwakilishi wake Bw. Kizito Wangalwa wameonesha kuguswa na tukio hilo. Mh. Sospeter amewaomba wanafamilia na jamii yote ya shuleni hapo  kuwa wavumilivu kwani taifa limepoteza nguvu kazi ya taifa na kizazi tegemezi.

Pia mbunge wa eneo hilo Mh. John Bunyasi amewaomba wazazi wasisitishe kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria ziara hizo kwa sababu ya vifo hivyo, bali amewaambia ziala kama hizo za kielimu ni muhimu sana katika kujifunza mambo mbalimbali ya msingi.....namnukuu alisema:"Such tours are important because they expose our children to the outside world,"

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika nyumba maalumu ya kuhifadhia maiti "Tanaka Nursing home mortuary".

No comments: