Shughuli ya ukusanyaji wa makopo ya maji/juice na plastic materials kama plastic chairs, galons na baadhi ya vifaa vya material hayo imekua kwa kasi kubwa sana kwa baadhi ya wakazi wa mjini. Pia shughuli hiyo imesaidia kutoa ajira kwa baadhi ya vijana ambao
wamekuwa wakikusanya hizo galons na kupeleka sehemu husika kwa ajili ya
kufanyiwa recycling kwa kuzalisha bidhaa nyingine. Taka hizo maranyingi huwa zinahifadhiwa kwenye mifuko mikubwa ama kwenye nyavu maalumu walizozishona wao kulingana na ukubwa wa mzigo wanaohitaji wao katika kuhifadhi.
Kwa hakika kabisa shughuli hii ilianzia kwenye baadhi ya miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza na Arusha ili kuweka jiji katika hali ya usafi. Vilevile shughuli hii imekua haraka kwa sababu ya kuwepo kwa baadhi ya viwanda vinavyofanya kazi ya recycling hapa nchini..kwa mfano kipo kiwanda mkoani Morogoro ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 2004/2005 kama sijakosea, kiwanda hicho kilianzishwa kwa nia ya kutengeneza mifuko ya plastic almaarufu kama mifuko ya rambo. Hadi hivi sasa kimeongeza uzalishaji wa bidhaa na kuzalisha plastic material zingine kama viti vya plastic meza na baazi ya bidhaa zingine za plastic. Sasa kama uzalishaji umeongezeka, ni kwanini vijana wengi wasijiongeze katika swala la ukusanyaji/uokotaji wa chupa hizo?
Hii ndio imenifanya nijiulize na kujaribu kupeleleza "hivi ni kwanini wanaofanya shughuli hii ya ukusanyaji makopo hayo hususani wale wakusanyaji wadogowadogo wanaokusanya mitaan ni wana matatizo ya akili au ni wale walevi walevi wa pombe za kienyeji?". Kwa mujibu wa wahusika wa shughuli hiyo ya ukusanyaji wa taka hizo ama plastic hizo zilizokwishatumika, wamesema huwa inawalazimu wawatumie vijana ambao wanaweza wakajituma kutembea juani, kuingia majararani na baadhi ya sehemu ambazo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuweza kufanya hivyo, na hii inatokana na malipo ya shughuli hiyo kwa wakusanyaji wadogowadogo kuwa ya kiasi cha chini sana. Wanasema huwalipa wakusanyaji hao kwa kiasi cha shilingi 300 hadi 600 kwa kujaza kiroba kimoja, pia inategemea na kilo za ujazo wa hicho kiroba.

Hapa kopo zikiwa zimekusanywa ila bado hazijahifadhiza
Chupa zimewekwa kwenye nyavu maalumu
Haya ni maeneo ya kiwanja cha ndege mkoani Morogoro
Modeko-Morogoro
baadhi ya wakusanyaji wa chupa hizo
makala hii itaendelea....
No comments:
Post a Comment