Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa
katika ajali ya gari aina ya daladala inayosafirisha abiria kati ya
Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea
kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu ya injini.
Ilitokea saa saba mchana
december 30 katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta
cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo Iringa ambapo shuhuda wa ajali
amesema hii daladala ilikua inatokea Mwangata ilipofika sehemu ya tukio
alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la
kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria
wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima
moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha
ya kuungua na kuteketea kabisa.
Mmiliki wa dala dala Ayubu
Kabigi amesema amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo
lakini amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari
lake.
No comments:
Post a Comment