Monday, 10 December 2012

copy and paste

Naona imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa wasanii wamuziki wa hapa bongo kucopy swagga, rap-style, midundo na hata nyimbo nzima kwa kuibadirisha either lugha au kuiongezea baadhi ya mistari na kurecord.
Hivyo basi kwa sisi wapenzi wa muziki hatushangai kuona mfumo huu kutawala hapa bongo...mwanzoni ilikuwa kama ubunifu tu wa kuwafanya watu watoke kwenye game, na pia iliwafanya wasanii waoneshe vipaji walivyonavyo...lakini kwa sasa imekuwa kama ni gumzo na kuwashusha wasanii kwa muonekano wakutokuwa na uwezo binafsi. 
Pia wapo waliocopy na kuweka bayana kuwa wamecopy either beat,chorus, verse or rap-style toka kwa watu flani au muziki wa maadhi flani. Na pia wapo wanaocopy ila hawataki weka bayana kama wamecopy hadi hapo vyombo vya habari viwahadhiri na ndipo ukubali kuwa wamecopy.
Sasa leo nawapa aina mpya ya copy and paste: ni nyimbo mbili tofauti, na zimeimbwa na wasanii wawili tofauti...ila ni wakazi wa mkoa mmoja....
Anaitwa Nassa, video:Kila nabii
 Anaitwa Belle 9, video: Amerudi
 Hizi ni video mbili tofauti na waimbaji tofauti, ila wamejikuta wamevaa mavazi yanayofanana kimtindo...Siwezi sema wamecopiana kwa namna moja ama nyingine ila majibu wanayo wao wenyewe, ni idea tu nadhani zimekutana na kutoa kitu kama hiki...

1 comment:

Nuru said...

Iyo kaliiiiiii....