Wednesday, 28 September 2011

KIJANA ASIYE NA SKENDO CHAFU

 BELLE NINE
Baada ya kunywa SUMU YA PENZI ambayo ilimfanya awe mbali na MASOGANGE, akakutaarifu shabiki wake kuwa WEWE NI WANGU kabla ajakutana na lawama za Sheta akisema NIMECHOKWA, alishauriwa na Nikki Mbishi kwamba sio KILA SIKU awaachie wadeni wake ila awaambie NILIPE NISEPE...
Abedenago Damian almaharufu kama Belle 9, anayeiwakirisha vyema sana Moro-Town, alianza kuwika mwishoni mwa mwaka 2008 baada ya single yake ya sumu ya penzi iliyoteka nafsi za watanzania wengi haikubagua umri wala jinsia, sababu iligusa sana maisha halisi ya mwanadamu katika suala zima la mapenzi.
Belle 9 amekuwa shabiki mzuri sana wa watu sio tu wa mkoani kwake nikiwa na maana kwamba Morogoro, lah ila takribani Tanzania nzima na Afrika mashariki na kati. Sababu kubwa iliyomfanya apendwe sana na mashabiki wake ni kutokana yuko simple sana yaani hana tabia ya kujisikia kama wasanii wengine, pia amejitahidi kwa kiasi kikubwa sana kukwepa skendo mbalimbali ambazo zinawakumba wasanii wengi wabongo.
Jembe hilo la Moro Town, linampango wa kuachia album yake ya pili hivi punde baada ya ile ya mwanzo aliyoipa jina la sumu ya penzi..Hivyobasi mashabiki na wapenzi wa Belle 9 kuwenitayari kwa new album kutoka kwa askari anayeibeba Moro-Town.

No comments: