Friday, 13 August 2010

HIZI KAULI MBIU ZINAMAANA GANI?




Fiesta ilianzishwa mwaka 2000 na kituo maarufu cha utangazaji"CLOUDS FM" kipindi hicho kulikuwa na wasanii wanaotamba kwenye musiki huu wa bongo fravour kama Inspecta Halun, Crazy GK,Prof. jay,Solo thang, Jay moe, Soggy Dog, LWP, Manyema family, manduli mob na wengine wengi....lakini!!!!








Miaka ya hivi karibuni yaani 2005 hadi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye musiki huu wa kizazi kipya hususani kuwepo kwa bifu baina ya wasanii mfano mzuri ni bifu la kundi la East Coast Team na TMK, pia tumeona bifu la Afande Selle na O-Ten na wengineo..Pia mbali na mabadiliko hayo kumekua na maongezeko mengine mengi tukiona kwenye upande wa vyombo vya habari kuwa na vipindi vingi vya kurusha bongo flavour pia matamasha yameongezeka kupitia bongo flavour kwa mfano STREET MUSIC kupitia SM, VUNJA JUNGU, FIESTA kupitia CLOUDS FM anbao ndio wanaoongoza kuandaa matamasha makubwa hapa bongo wakiambatanisha na wasanii wakubwa kutoka nje mfano JALURE, BUSTA, LIL KIM..Pia wamekuwa na kauli mbiu mbalimbali mfano "FIESTA FULL SHANGWE (2006), FIESTA JIRAMBE. FIESTA ONE LOVE (2009) na FIESTA JIPANGUSE 'RRAAAA RRAA'(2010)..Je hizi kauli mbiu zina maana gani kwa jamii??

No comments: