Friday, 4 October 2013

Waumini wa kiislam wachezea risasi-Kenya

Kiongozi wa dini ya kiislam huko nchini Kenya, Sheikh Ibrahim Rogo na waumini wenzake  wanne waliokuwa kwenye gari wakitokea mskiti wa Musa wamejikuta wakichezea risasi za kutosha kutoka kwa kikundi cha watu waliodaiwa kuwa ni miongoni mwa kikundi cha kigaidi  cha AL-SHABAB kinachoisumbua Kenya hivi sasa.

Sheikh Rogo na jamaa zake hao wanne wamepigwa risasi umbali wa kilometa moja kutoka kituo cha polisi cha Bamburi, nchini humo wakiwa kwenye gari yao ndogo aina ya Toyota Fun Cargo baada ya watu wasiojulikana waliokuwa kwa miguu wakaanza kuwamiminia risasi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kimesema miongoni mwa jamaa  hao waliopoteza maisha hapo hapo ni shemeji wa marehem Gadaff ambaye dada yake aliolewa na Gadaff, Issa Abdalla aliyekuwa dereva wa gari hilo, wengine ni Gadaff Mohammed ambaye alidaiwa kuwa ni fundi wa Samani (furniture), Omar bu Rumeisa na Sheikh Salim ambaye alinusurika kwenye tukio hilo.

"Tumewamaliza", Sheikh Salim Aboud aliwasikia wakisema hivyo baada ya yeye kujifanyisha kama amekufa, na kisha watu hao wakaingia kwenye gari aina ya Mark X na kuondoka eneo hilo.

Mmoja wa kiongozi wa dini hiyo ya Kiislam, Sheikh Aboubakar Sheriff maarufu kama Makaburi ambaye aliwasiri katika eneo la tukio, alikilaumu kikundi cha polisi kinachojihusisha na kutokomeza ugaidi (ATPU) "Anti Terrorism Police Unit"... Amesema "hao ATPU wapo hapa, kwanini wahusika wamekimbia? tutafanya kipi sasa na kwanini wanatuua? Hatujaua hata mmoja lakini polisi wanawaua waislam wasio na hatia"...alisema Sheikh Makaburi.

Kwa mujibu wa Sheikh Ibrahim ambaye hakuwepo wakati wa shambulio la Westgate...amesema "tukio hilo limefanywa na wamerekani na waisrael, kwanini serikali ya watu wa magharibi hawataki kabisa waislam tuzungumzie kuhusu Jihad?", hii ni sehemu ya kutuangamiza na kutuua sisi sote".

No comments:

Post a Comment