Thursday, 3 October 2013

Hatimae Water na 20% wamaliza tofauti zao

Hatimae msanii aliyekinukisha kwenye Tuzo za Killi mwaka 2011 baada ya kuongoza kwa kunyakuwa tuzo tano kwa mpigo, 20% ambaye pia ni msanii pekee mwenye uwezo wa kutoa nyimbo zenye ujumbe wa kuielimisha jamii na pia naweza kusema ni miongoni mwa wanamuziki wenye muonekano tofauti na kazi wanayoifanya. Habari iliyotufikia inasema kuwa msanii huyo amefanikiwa kumaliza tofauti zao na producer wake Man Water aliyeweza kumfanikishia jamaa kunyakua tuzo hizo tano.

Man Water, ni miongoni mwa watayarishaji wanaofanya vizuri hapa Bongo na kuweza kuinua n kuendeleza vipaji vya muziki kwa baadhi ya wasanii wachanga na walio kwenye game hii ya muziki huu wa kizazi kipya. 

Water na 20% walikuwa na tofauti zao ambazo chanzo hakikuweza kuzitaja zaidi ya kusema kuwa ni tofauti zao wenyewe wanajua, hivyo wameamua kumaliza tofauti hizo na kufanyakazi tena pamoja... 

No comments:

Post a Comment