Sunday 13 October 2013

Jay Z, Chriss Martin na Timberland wawashangaza wadau kwa kujimix kwenye treni ya abiria

Hii imetokea juzi (Jumaamosi) huko jiji London baada ya wakali hao wa muziki ulimwenguni kujikuta wanakwea treni la abiria bila kujistukia na kufika wanapotakiwa kwa ajili ya kufanya show.
Jay Z ni miongoni mwa wanamuziki wenye mafanikio makubwa sana hasa katika suala la mkwanja mbapo angeweza kufanya kitu chochote kile anachokitaka katika hii dunia ambacho kinatengenezwa na binadamu... hilo kwake hakujali akaamua kukaa kwenye kituo cha treni za abiria wa kawaida kusubiria treni ije waanze safari yao kama kawaida.
Kitendo hicho kimezua mjadala mkubwa hususani kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo twitter baada ya wadau kupost ujumbe unaoonesha kushangazwa na kitendo walichokifanya mastaa hao kwa ni kitendo ambacho si cha kawaida kwa mastaa kama hao kukifanya.

No comments: