Wednesday 17 April 2013

mafuriko yauwa watoto nchini Kenya

Watoto wawili wapoteza maisha baada ya kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha nchini Kenya. Watoto hao ambao ni wakazi wa kijiji cha Narok - Magharibi mwa Kenya wamesombwa na mvua hiyo wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya wazazi wao katika kijiji hicho. Mvua hiyo iliyoambatana na matope mazito yaliyosababisha kuziba kwa baadhi ya mifereji na kuleta maafa makubwa.

Kwa kawaida kwa nchi hiyo ya Kenya kuwa na mvua kali kwa kipindi hiki kwani mara nyingi mwezi March mbaka May huwa kuna mvua za namna hiyo. Polisi wakiongea na BBC leo wamesema mvua kubwa iliyonyesha mwezi huu nchini humo imeleta maafa makubwa kwa wakazi wa nchi hiyo kwani imesababisha watu zaidi ya 36 wamepoteza maisha na 52,000 wajeruhiwa, pia imesababisha kuharibu makazi ya watu na baadhi ya vitu kupotea.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema mafuriko hayo yameharibu barabara na baadhi ya maeneo yameharibika kabisa. Pia amesema miongoni mwa barabara zilizoharibika ni barabara kuu inayoiunganisha Kenya na Uganda.

Siku ya jumatatu, Kenya's Deputy President "William Ruto" alisema serikali imeshatoa kiasi cha fedha ($ 18m) kwa ajili ya ukarabati wa uharibifu huo na kwa waathirika wa maafa hayo.

No comments: