Tuesday, 26 March 2013

"Love & Power" ya kanumba yaingia sokoni april

Filamu mpya ya ''Love & Power'' ambayo ndio baadhi ya kazi za mwisho za msanii hayati Steven Charles Kanumba, ambapo yumo pia marehemu Sharo Milionea, inatarajiwa kuingia sokoni baada ya msambazaji wa filamu hiyo kuikamilisha na kusema kuwa filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwezi April baada ya kuzinduliwa kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni… Filamu ya ''Love & Power'' ni kazi ya pekee kuigizwa na msanii huyo kabla ya umauti kumfika, ni filamu aliyorekodi siku za mwisho kabisa… Filamu hiyo ambayo wengi wanasema marehemu Kanumba alijitabiria kifo chake, itazinduliwa sambamba na kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwake, April 7 2012… Akizungumza kupitia EATV hii leo, mdogo wa marehemu Kanumba ambaye pia ni kiongozi wa ofisi ya ''Kanumba The Great'' iliyopo Sinza-Mori, Seth Bosco, alisema zaidi ya waigizaji 10 kutoka Ghana wanatarajiwa kuwepo siku hiyo… Alisema mbali na waigizaji hao wa Ghana, pia rafiki wa marehemu, ambaye ni muigizaji maarufu barani Afrika kutoka Nigeria, Ramsey Noah pia anatarajiwa kuwepo siku hiyo ya uzinduzi… Akizungumzia ratiba ya siku hiyo, Seth Bosco alisema itaanzia nyumbani kwa marehemu, baada ya hapo wataelekea makaburini Kinondoni na baadaye Leaders Club kwa ajili ya uzinduzi huo

No comments:

Post a Comment