Tuesday, 26 March 2013

Angelina Julie atua africa

Angelina Jolie
Muigizaji wa Hollywood Angelina Jolie yupo barani Afrika kuendelea na majukumu yake kama mwakilishi maalum wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR na anazitembelea DR Congo na Rwanda… Angelina anasafiri na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Wiliam Hague, na atakutana na wanawake na wasichana waliokumbana na vitendo vya ubakaji. Makundi ya waasi na wanajeshi wa Congo wamekuwa wakituhumiwa ubakaji… Kwa mujibu wa ofisi ya Hague, lengo la safari hiyo ya Congo na Rwanda, ni kukutana na waathirika wa ubakaji na ukatili wa kimapenzi pamoja na kukutana na viongozi wa kisiasa kujadili suluhisho la mgogoro huo

No comments:

Post a Comment