Monday, 25 March 2013

wema amtoa kajala jela

Wema na Kajala kwenye moja ya vipande vya filamu
walizowahi kucheza kabla ajaenda selo
Goodo news kwa mashabiki wa muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200. Taarifa kutoka mahakamani zinadai kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga fedha hizo ili wazilipe na uhakika wa kwenda nyumbani kwao ni mkubwa. Mrembo huyo na mumewe Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni pamoja na kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam. Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment