Friday 29 March 2013

dar: "why always me?"

Jiji la Dar es salaam limekuwa na maafa yenye kuua takribani watu wengi sana kwa matukio ambayo hayana majibu kwa jamii na serikali kwa ujumla. Tunakumbuka mwaka 2002 kuna maafa yalitokea bahari ya Hindi yaliyojulikana kwa jina la "TSUNAMI" na kuua watu kadhaa wa jiji la Dar es salaam.
Mbali na tukio hilo likaja la mabomu ya Mbagala ambayo nayo yaliua watu wengi tu tena wasio hata na hatia, achana na hilo likaja la Gongo la Mboto pia wakafa wananchi wengi tu wasio na hatia....
athari za mabomu- gongo la mboto
Yote tisa...kumi la mafuriko yaliyoiwekea historia jiji la Dar es salaam kwa kuua watu zaidi ya 200 na kuwafanya baadhi ya wananchi wakose mahali pakuishi hadi leo.
athari za mafuriko - Dar(2011)
Leo hii majira ya saa tatu asubuhi yametokea maafa mengine yaliyoteketeza maisha ya watu waliokuwepo katika eneo hilo. Ambapo jengo lililokua bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indra Gadhi na morogoro lenye ghorofa zaidi ya 14 limedondoka wakati likendelea na ujenzi na kuangukia msikiti ambao unasadikiwa kuwa na madrassa ambayo kulikua na wanafunzi ndani wakati wa tukio, Chanzo cha habari kimeripoti kuwa inawezekana zaidi ya watu 60 wamefunikwa na jengo hilo. Mbaka tunapata habari hizi ni kwamba zaidi ya maiti 18 zilikuwa zimetolewa kwenye jengo hilo na zaidi ya majerui 22 waliwahishwa hospitalini kwa matibabu.

Baadhi ya viongozi na wanausalama wamefika eneo la tukio, pia rais Jakaya Kikwete mchana huu ametembelea eneo lilipoanguka jengo hilo na kuhimiza juhudi za uokoaji ziongozwe ili kuokoa maisha ya watu wanasadikiwa kuwa wapata 60 waliofukikwa ndani ya Kifusi.Tayari askari wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) na lile la Wananchi(JWTZ) wapatao 500 wako eneo la tukio katika juhudi za uokoaji.

baadhi ya picha za tukio hilo

 Mkuu wa mkoa Said Meck Sadick akiwa na Rais Kikwete na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, wakiwa wanaangalia jengo lililo dondoka
 hii ni taswira ya juu
juhudi za uokoaji zikiendelea

No comments: