Wednesday 27 February 2013

q-chief apanda steji moja na baba yake mzazi

Msanii Q-chief au ukipenda muite Q-Chillah a.k.a Savimbi, juzi alikamua vya kutosha ndani ya club maisha.
Chillah alikamua baadhi ya nyimbo zake zilizoweza kutamba miaka ya nyuma kama vile Sex, Tanita, Ma Boo, Waiper, Mariam, na nyingine nyingi ambazo ziliweza kuzikonga nyoyo za wadau na wapenzi wa Q Chief waliokuwepo kwenye show hiyo na kuweza kudhihirisha kuwa yeye bado Legendary kwenye game ya Bongo Fleva.
Hivyo basi Chilla katika kudhihirisha ya kwamba kipaji si cha kubabaisha au cha kufoji kama wasemavyo waswahili, aliamua kupanda na baba yake mzazi na kuweka bayana kwamba hana bifu na baba yake kama ilivyojulikana hapo awali baada ya kutoa nyimbo ya Si ulinikataa kipindi cha nyuma wakati anaanza kutoka kwenye game ya bongo fleva.
Watu walihamaki na kushangilia vya kutosha kwa kitendo alichokifanya msanii huyo kwa kupanda na mzee wake kwenye steji.
 Q-Chillah akikamua
 Hapa Q-Chillah akiwa na baba yake mzazi stejini

No comments: