Saturday 23 February 2013

miaka mitatu sasa jakaya hajajibu barua ya papii kocha

Mwezi na tarehe kama ya juzi (tarehe 21) mwaka 2010, Papii Kocha alimuandikia barua rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete angalau awapunguzie hadhabu waliyonayo huko gerezani yeye na baba yake mzee Nguza Viking.
Mbali na Kuachiwa kwa baadhi ya watoto wa familia hiyo ya mzee Nguza waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, Papii na baba yake bado wanaendelea kutumikia kifungo hicho hadi sasa, hii inadhihirisha kuwa Mh. hajaweza kuamua kitu juu ya barua aliyoandika Papii Kocha ya kumtaka awapunguzie hadhabu inayowakabiri.
Hii ndio barua aliyoiandika Papii Kocha kwa rais;
Barua aliyoiandika Papii Kocha
 Papii Kocha na baba yake mzee Nguza wakirudishwa baada ya kusikiliza kesi yao inayowakabiri baada ya kushindikana kwa kukatiwa rufaa (2010)
BARUA YENYEWE INASOMEKA KAMA IFUATATAVYO:

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.

Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu

Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki

Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

Na huo ndio mwisho wa barua aliyoiandika Papii ili imfikie Mh. Rais

source and special thanks to: Ladyjaydee blogspot

No comments: