Wednesday 11 April 2012

LULU AMEPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Leo Jumatano 11/4/2012 - Mwigizaji wa movie za kitanzania
 ELIZABETH MICHAEL maarufu kama Lulu mwenye umri wa miaka 17
 mkazi wa Tabata, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya 
Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yanayomkabili kuhusu mauaji 
ya msanii mwenzake wa maigizo STEVEN CHARLES KANUMBA.
Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili ElizabethKaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.
Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

No comments: