Monday 24 March 2014

New Hit:Sina Gari-Jaggar ft Empress

Ujio mpya kutoka kwa Jaggar akiwa na mwanadada Empress kutoka Kenya, wimbo unaitwa Sina gari unaeleza mtu wa hali ya chini kumpenda mwanamke wa hali ya juu...kutokana na hali hiyo jamaa anakumbana na changamoto nyingi kama kutukanwa, kudharirishwa na mwisho wa siku anaamua kutumia njia ya uongo ili aweze mshawishi mwanadadashosti na kuweza kumpata. Wimbo umetayarishwa na producer Saya B. Video iko katika hatua za mwisho za kumaliziwa kushoot na editing kadhaa ila audio imeanza kusambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii japo bado haijaachiwa officially.

"Hii ni project ambayo itakuwa inaendelea hivi kwa kila mwezi tofauti na awali nilikuwa naachia wimbo mmoja kwa mwaka kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wangu kwa kuwa nilikuwa busy na masomo...kwa sasa nipo free na ndio project inaanza now, so kaa tayari".....

"Nimeshafanya track kadhaa na kuziachia japo hazikuweza fanya vizuri kihivyo....nilifanya track na Beka "My Baby", "Sauti zetu" nikiwa na Belle 9 na "Some days" nikiwa na Bupe."....amesema Jaggar

No comments:

Post a Comment