Pata kumfahamu kijana mwenye asili ya kisomalia aliyekuwa nominated kwenye Oscar, Barkhad Abdi kijana mwenye umri wa miaka 28. Pia fahamu ni kwanini aweze kuwa kivutio na ni kishawishi kikubwa kwako??
Kisomalia jina laki linatamkwa "Barkhad Cabdi", na kwa kiarabu linatamkwa برخد عبدي;
Barkhad alizaliwa miaka 28 (April 10, 1985) iliyopita huko Mogadishu, Somalia ambako aliishi na kukulia huko mbaka miaka saba (7) na kisha kuhama makazi baada ya vita ya kikabila iliyokuwa ikiendelea nchini humo. Barkhad na familia yake walihamia Yemen kama wakimbizi ili kuwa salama dhidi ya mapigano yaliyojili huko Somalia.
Hata hivyo kwenye mahojihano mbalimbali, Barkhad amekuwa akielezea maisha yake tangu alipoanzia na mbaka sasa alipo ni kuwa amekulia kwenye vita.
“I have good memories and bad memories of Somalia.
You know, I remember the peaceful days, the beautiful Mogadishu. I
remember when the war happened — overnight. Dead
people everywhere and gun shots don’t stop,”.
"ninayo kumbukumbu nzuri na mbaya pia kuhusu Somalia. Unajua, nakumbuka zile siku za amani, uzuri wa Mogadishu. Nakumbuka kipindi vita inatokea, usiku mzima. Watu walikufa kila mahali na bunduki kupigwa bila kusimama," alisema kijana huyo.
Kutokwenda shule ya msingi ni matokeo ya kuwa mkimbizi huko Yemen, hivyo basi alijiingiza kwenye mchezo wa bahati nasibu ambao ulimuwezesha kubahatika na kuweza kushinda kadi ya kijani iliyompa safari ya kuweza kuingia Marekani akiwa na umri wa miaka 14. Hivyo basi mnamo mwaka 1999 aliweza kuhamia Minneapolis, nchini Marekani akiwa na familia yake na kuweza kujiunga na chuo cha Minnesota State University Moorhead kilichopo umbali wa takribani masaa manne na walipokuwa wanaishi (Minnieapolis).
Kabla ya kujiunga kwenye suala zima la uigizaji wa filamu, Barkhad alikuwa akifanya kazi mbalimbali ikiwa pamoja na kuendesha Tax kabla ya kuwa Abduwali Muse kwenye Captain Phillips.
Kabla ya kujiunga kwenye suala zima la uigizaji wa filamu, Barkhad alikuwa akifanya kazi mbalimbali ikiwa pamoja na kuendesha Tax kabla ya kuwa Abduwali Muse kwenye Captain Phillips.
Kilitokea nini hadi Barkhad kuwa star?:
Mwaka 2013 Barkhad Abdi aliweza kucheza filamu iliyofahamika kwa jina la Captain Phillips, akiwa kama muhusika mkuu kwenye filamu hiyo aliyetumia jina la Abduwali Muse. Aliweza kuwa mgombea tuzo kwenye tuzo za Screen Actors Guild kama the Best Supporting Actor. Pia alichaguliwa kugombea tuzo za Academy Award kama Best Supporting Actor. Mbali ya tuzo hizo pia Abdi amechaguliwa kuwania tuzo ya Golden Globe Award na BAFTA Award kama Best Supporting Actor. Kwa uzoefu alioupata kwenye Captain Phillips ambayo ni filamu yake ya kwanza, baada ya kuwa nominated kwenye tuzo hizo, amejitengenezea monekano wa mara nyingi kwenye vyombo mbalimbali vya habari dunia kote na kumfanya awe star. Mwanzoni mwa mwaka 2014, Abdi alisema amepanga kuhusisha maeneo ya Los Angeles katika filamu yake anayoi'direct, Ciyaalka Xaafada. Pia amedirect video mbalimbali za muziki kama alivyozisoma mwezi January 2014 alipokuwa akisoma scripts za TV show.
Tuzo anazowania Barkhad:
Kwa upande wa kuchaguliwa kwake kuwa mshiriki wa tuzo ya Oscar, Barkhad Abdi amechaguliwa kuwania tuzo ya Golden Globe, na tuzo ya SAG na BAFTA.
Je, ni nini kiwe kishawishi kwako kuhusu maisha ya Barkhad?:
Tunaweza kusema kuwa, kutokana na wanadamu wengi hususani sisi waafrika tuliozaliwa na kukulia kwenye maisha duni nikiwa na maana yale maisha ya hali ya chini sana kwenye suala zima la kipato cha mzazi au mlezi hata sisi wenyewe pia, na ikitokea hukubahatika kupata elimu yeyote ile, basi tunajikuta kukata tamaa ya maisha na kuvunja ndoto zetu na kujikuta kuwa watenda maovu bila kutarajia. Kumbe iko tofauti na matakwa yake Allah/Mwenye Mungu, kwa maana yeye ndiye ajuaae nani ataishi vipi, na ni yupi atafanikiwa kwenye maisha haya, na pia ni nani mwenye kuweza kuendeleza ndoto alizomjaliia yeye Allah kwa namna yeyote ile kana kwamba iwe amesoma au hakusoma, awe amezaliwa kwenye hali duni kimaisha au hali nzuri kimaisha.
Hivyo napenda kukusihi ewe kijana usivunjike moyo hata kama hukubahatika kuzaliwa na maisha mazuri au kutokwenda shule, muombe Mungu uenda siku moja kila kitu kitakuwa sawiha kama ilivyotokea kwa kijana Barkhad Abdi.
No comments:
Post a Comment