Thursday, 6 March 2014

Hatimaye Kanye na Kim watangaza siku ya ndoa yao

Kanye West na mchumba wake Kim Kardashian wametangaza siku yao ya kufunga ndoa baada ya kuvishana pete mwezi Oktoba. Wapenzi hao wenye mtoto wa miezi 8, "North" wameweka wazi kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwezi May tarehe 24 huko Paris, nchini Ufaransa kwamujibu wa mtandao wa Us Weekly.

Kanye West na Bibie Kim wamesema wameamua kufanya party ya ndoa yao huko Paris, Ufaransa kwa kuwa ndio sehemu ya makazi yao kwa sasa mbali na makazi yao ya mwanzo yaliyopo huko Marekani. Hata hivyo ndoa hiyo haitakuwa kubwa kwani wanataka kuifanya ya kawaida sana tofauti na wanavyotarajia watu.

No comments: