leo tarehe 04th March ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mmoja wa watu maarufu sana wa bara la watu weusi "Afrika", Miriam Makeba maarufu kama Mama Africa.
Miriam Makeba alizaliwa miaka 82 iliyopita (4 March 1932) na kufarika miaka 6 iliyopita (9 November 2008). Mama Africa, aliweza kushinda tuzo za Grammy Award kama mwimbaji kutoka South African na civil rights activist.
Miaka ya 1960's, alikuwa mwanamuziki/msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika kuweza kuwahamasisha muziki wa waafrika ulimwenguni. Aliweza kufahamika hasa kwa kupitia wimbo wake wa "Pata Pata", ambao aliurekodi mwaka 1957 na kuuachia huko Marekani mwaka 1967. Aliweza kurecord na kupata ziara na wasanii wengi wakiwemo, Harry Belafonte, Paul Simon, na mumewe wa awali Hugh Masekela.
Makeba pia alishiriki pia kwenye kampeni za kutokomeza ubaguzi wa rangi "Apartheid" uliokuwa ukiendelea nchini Afrika ya kusini. Serikali ya Afrika ya kusini ilisitisha passport yake mwaka 1960 pamoja na uraia wake 1963 alikimbia nchini mwake na kurudi mwaka 1990 baada ya kutoweka ubaguzi wa rangi kwa jitihada za hayati mzee Nelson Mandela aliyekuwa rais wa kwanza nchini humo.
Makeba alifariki kwa mshtuko wa moyo mnamo tarehe 09 November 2008 baada ya kuperform kwenye tamasha lililoandaliwa kumsupport mwandishi Roberto Saviano dhidi ya Camorra.
No comments:
Post a Comment