Mwanafunzi wa chuo cha Cape Coast aliyefahamika kwa jina la Godwin Awogbo amekutwa akiwa amekufa nje kidogo na campus ya chuo hicho siku ya Jumaatano (Tarehe 19)
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii "PeaceFmOnline.com" kiliweza fanya mahojihano na shuhuda wa tukio hilo na kuweza kutambua kuwa kijana aliyeuwawa katika eneo hilo la chuo ni mwanafunzi wa chuoni hapo. Shuhuda alisema..."huyu ni mwanafunzi na alikuwa akisoma chuoni hapa akichukua kozi ya Social Science hii ni kwa mujibu wa rafiki yake ambaye walikuwa wanakaa wote chumba kimoja, roommate wake amesema alijaribu kumpigia simu rafiki yake Godwin baada ya kuona amekuwa nje ya hostel kwa muda mrefu, ghafla hakuweza kumpata hadi hapo asubuhi alipopokea taarifa kupitia simu yake kwa njia ya meseji na kutaarifiwa kuwa kuna mwili wa rafiki yake aliyekuwa amekwisha fariki".
Sababu zilizopelekea kifo cha mwanafunzi huyo bado hazijaweza kubainika na mbaka sasa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya kifo cha mwanafunzi huyo. Pia polisi wameweza kuhusisha taarifa zingine juu ya kupatikana kwa mwili wa kijana huyo jirani na hotel ya Brown Palace iliyo karibu na chuo hicho.
No comments:
Post a Comment