Tuesday 21 January 2014

Wolper amuanika mchumba wake mtandaoni

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.

Huu ndio ujumbe wa Wolper.

'“Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.

Wolper aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja kwa wazazi wa pande zote mbili ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha...

No comments: