UONGOZI wa Yanga umemhakikishia kocha, Ernest Brandts, kwamba
kibarua chake kipo salama, lakini kocha huyo ametaja mambo
yaliyosababisha kikosi hicho kilichosheheni mastaa ghali kupata kipigo
cha aibu kutoka kwa Simba katika mechi ya Mtani Jembe juzi Jumamosi.
Simba iliichapa Yanga kamili mabao 3-1, mabao ya Simba yalifungwa na Amissi Tambwe (mawili) na Awadh Juma, wakati Emmanuel Okwi ndiye aliyeifariji Yanga.
“Tumefungwa ni kweli, hakuna atakayebisha juu hilo na uwezo tuliouonyesha, wachezaji wa Yanga sasa kila mmoja anajiona ni staa, hakuna aliyeko chini ya mwenzake. Hilo ni tatizo katika timu na ni kitu cha kwanza kilichochangia kufanya vibaya,” alisema.
Alisema kikosi chake hakikucheza kitimu na ndiyo maana muda mwingi hawakuweza kutatua matatizo yaliyokuwa yakijitokeza uwanjani wala hawakuelekezana jambo la kufanya kwa wakati.
Wachezaji wote hao walikuwa wakizichezea timu zao katika Kombe la Chalenji lililomalizika siku 10 zilizopita. Deo Munishi alikuwapo Chalenji lakini hakuchezeshwa mchezo huo.
Luhende alishindwa kumkaba Amissi Tambwe asifunge bao la kwanza kwani aliingia kati kukaba na alishindwa kumzuia haraka Ramadhan Singano ‘Messi’ hadi akamkwatua ndani ya eneo la hatari na kusababisha penalti iliyozaa bao la pili. Yanga walikuwa na mategemeo makubwa ya kushinda mchezo kutokana na kuwa na wachezaji wengi wazoefu akiwemo staa mpya, Emmanuel Okwi ambaye anasifika kwa kucheka na nyavu.
Source:Gazeti la Mwanaspoti.
No comments:
Post a Comment